Wakati mjakazi akileta ujumbe wa mume wangu mpendwa alipokuwa anaanguka kwa miguu yangu na kuomba, mimi kwa kiburi changu hata sikumtazama au hata kusema naye.
Marafiki zangu walikuwa wakinishauri kwa maneno matamu lakini, nilikuwa nikiwajibu kwa kiburi na kuwafukuza.
Kisha, wakati Bwana mpendwa mwenyewe alikuwa akija na kuniita-Ewe mpenzi! 0 mpendwa! Nilikuwa nikinyamaza ili tu nijisikie muhimu.
Na sasa ninapoteseka na uchungu wa kutengana na mume wangu, hakuna hata mtu anayekuja kuniuliza ninaishi katika hali gani. Nikiwa nimesimama kwenye mlango wa mpenzi wangu ninalia na kuomboleza. (575)