Kichwa kiko juu ya sehemu zingine zote za mwili lakini hakiabudiwi. Wala hayaabudiwi macho yanayoona mbali.
Masikio hayaabudiwi kwa uwezo wao wa kusikia wala pua kwa uwezo wao wa kunusa na kupumua.
Mdomo unaofurahia ladha zote na usemi hauabudiwi wala mikono inayorutubisha viungo vingine vyote.
Miguu ambayo haina uwezo wa kuona, kuzungumza, kusikia, kunusa au kuonja inaabudiwa kwa sifa zake za unyenyekevu. (289)