Kama vile mshale unavyowekwa kwenye upinde, kamba ya upinde huvutwa na mshale kutolewa kuelekea upande unaokusudiwa kwenda.
Kama vile farasi anavyopigwa mijeledi ili kukimbia kwa kasi na kufadhaika, anaendelea kukimbia kuelekea anakoelekezwa.
Kama vile kijakazi mtiifu anavyoendelea kusimama machoni pa bibi yake, naye huharakisha kwenda mahali anapotumwa;
Vile vile mtu hutanga-tanga katika ardhi hii kwa mujibu wa matendo aliyoyafanya (katika kuzaliwa hapo awali). Anaenda mahali ambapo amekusudiwa kujiendeleza. (610)